|
||||
ADA ZA UANACHA - 2007
aribu Katika Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi
Asante kwa kutumia muda wako kutembelea tovuti yetu. Mwaka 2006 kwa msaada wa wanachama zaidi ya 250 na washirika wengine kutoka nchi mbalimbali 61, Umoja wa Kimataifa wa Wadau wa Mbuzi uliendelea kuhamasisha utafiti na maendeleo ya mbuzi duniani kote. Mwaka 2007 umoja huo unaadhimisha mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwake. Umoja unajivunia mafanikio uliyoyapata na ndani ya kipindi cha historia yake. Umoja unawategemea sana wanachama wake wenye ujuzi wa aina mbalimbali na uzoefu wa muda mrefu kama wewe kutimiza majukumu yao kwenye umoja huu, jamii zao, nchini mwao na duniani kwa ujumla. Tutaendelea kupanuka na kuboresha juhudi zetu za awali. Jiunge leo na utasaidia kuhakikisha kuwa juhudi zetu zinaangaza umuhimu wa mbuzi katika kuboresha maisha ya watu duniani kote kwa miaka mingine 25 ijayo. Hivi sasa tunajiandaa kwa Kongamano la tisa (9) la kimataifa kuhusu mbuzi ambalo litafanyika mjini Queretaro, Mexico, tarehe 31 agosti hadi tarehe 4 Septemba mwaka 2008, tunaamini kuwa unaweza kutusaidia kufanya Kongamano hili liwe na mafanikio makubwa. Moja ya malengo ya umoja wa wadau wa Mbuzi Kimataifa ni kuhakikisha kuwa wanataaluma mbalimbali vijana na hasa wanawake wanaopenda maswala ya utunzaji/uzalishaji na utafiti wa mbuzi wanashiriki katika Kongamano hili. Hivyo tunahitaji msaada wako ili kuweza kuwadhamini baadhi ya wanataaluma vijana ambao hawataweza kumudu gharama za kushiriki Kongamano hili. Wastani wa gharama zinazohitajika kudhamini ushiriki wa mwanataaluma mmoja kijana ni dola za Kimarekani elfu moja na mia tano ($ 1,500) ambazo zitatumika kwa kugharamia usafiri wa ndege, chakula na malazi. Tafadhali saidia kudhamini wanataaluma vijana: Ili kujifunza zaidi bofya hapa. Wenu Chris Lu Raisi wa Chama cha wadau wa mbuzi Tuesday, September 16th 2008
Camillus Ahuya, IGA Country Representative - Kenya
Article read 1647 times
Inside IGA -Who we are, what we do ! | Membership | Information on goats | Conferences | The goat products | Small Ruminant Research | Newsletters | L'IGA en Français | IGA in Turkish | IGA in Swahili | La IGA en Español | L' IGA en Italiano | A IGA no Portugues | The IGA in Persian |
In our store
|
|||
|
International Goat Association 12709 Grassy Drive, Little Rock, AR 72210, USA,
Tel : 1 501-251-9391 - Fax: 1 501-251-9391 admin@iga-goatworld.com - Web master: Christian K. De Vries All rights reserved |
||||





Inside IGA -Who we are, what we do !



